Tigo Kili Half Marathon | Tigo Tanzania

 Tigo Kili Half Marathon

Kampuni ya Tigo ambayo inaongoza kwa maisha ya kidijitali kwa mara nyingine inadhamini mashindano ya riadha ya Kilimanjaro Half Marathon yanayotarajiwa kufanyika Jumapili Februari 26 mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro. Huu ni mwaka wa tatu mfululizo kwa kampuni hiyo ya simu inayokua kwa kasi kutoa udhamini wake kwa tukio hilo maarufu la mwaka ambalo hukutanisha washiriki kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na hata nje.

Kuhusu ya Babu

Joram Mollel amezaliwa mkoani Arusha na amekulia kwenye kijiji cha Kijenge. Akifanya kazi kampuni ya Mgambo kama Mlinzi, Alikuwa na nia ya Kukimbia mbio ndefu kwenye riadha. Baada ya miaka mingi ya kushuhudia wanaridha wengine, Hatimaye Joram Mollel alijiunga na kikundi kimoja cha riadha. Kuanzia hapo, Mazoezi yake endelevu yalimfanya kushiriki mbio nyingi za riadha. 

Kuhama makazi yake mara kwa mara kulipelekea kupoteza picha zake nyingi, historia ambayo anakosa ukumbusho wake.Juhudi daima, Joram Anasonga mbele na kutujulisha ni jinsi gani riadha ni sehemu ya maisha yake. Sio tu Kujipa nguvu kwa kupitia riadha bali nguvu inayo msaidia kufanya shughuli zake za kila siku kwa faraja.

 

 

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo