Tigo Pesa FAQs | Tigo Tanzania


Tigo Pesa FAQs

Ndio, haijalishi mtandao gani unatumia. Hakikisha wakati unajisajili na app ya Tigo Pesa laini yako ya Tigo iko kwenye simu unayotumia na unatumia intaneti ya Tigo na sio mtandao mwingine, baada ya kujisajili ndo unapoweza kutumia mtandao mwingine.

Ndio, utatumia namba ya siri ile ile unayotumiaga ukipiga *150*01#. 

Huduma zote za muhimu ambazo zipo kwenye Tigo Pesa zinapatikana katika app ya Tigo Pesa.

Mteja anaweza pakua app kwa kutembelea App Store au kwa kubofya kiungo itakayotumwa kwa SMS au tembelea tovuti yetu ya Tigo kupakua App.

Hatushauri wafanyabiashara kutoa pesa kwasababu wanaweza kufanya shughuli mbali mbali na hela iliopo kwenye akaunti, unaweza fanya ifuatavyo.

  • Unaweza kuongeza bidhaa zako kwakulipa wasambazaji waliojisajili.
  • Unaweza kuhamisha salio la hela kwenda kwenye akaunti ya benki.
  • Unaweza kulipia bili tofauti zilizopo kwenye menyu ya Tigo Pesa.
  • Unaweza hamisha hela kutoka akaunti ya Tigo Pesa kwenda kwa akaunti zingine.

Tumia akaunti yako kuokoa pesa ili upate gawio la Tigo Pesa kila baada ya miezi mitatu.

Tuna ushirikiano mzuri na vituo vyetu vya simu, tunawashirkisha habari zote kuhusu wafanyabiashara na hamna mabadiliko yanayofanyika bila idhini ya mfanyabiashara.

Ndio, pesa ilioko kwa akaunti ya Tigo Pesa inaweza patikana kwa ndugu pale mfanyabiashara akifariki, kwakkuwasilisha nyaraka zitakazotakiwa na kufuata utaratibu wa kawaida, kama cheti cha kifo nk.

Mara nyingi meseji ya kukamilika kwa muamala huingia baada ya muda mfupi lakini kuna muda mwingine mtandao unaweza kusumbua.

Kama umesubiri zaidi ya dakika 10 na hujapata meseji ya kukamilika kwa muamala, angalia salio au piga simu kwa kituo vyetu vya simu kwa kupiga 100.

Tigo Pesa inategema mtandao wa Tigo. Kwa bahtai mbaya ambapo mtandao wa Tigo utakua uko chini, epuka kufanya muamala wa aina wowote mpaka pale mtandao utakapo rudi hewani na ukiona simu yako ina mtandao.

Cha kwanza  ni kupiga simu kituo cha simu cha Tigo Pesa kwa kupiga 100 au tembelea duka lolote la Tigo Pesa na toa taarifa ya kupotea kwa laini au simu.

Mhudumu atakuuliza maswali ili aweze kuthibitisha uhalisia wa mteja na ndipo kuweza kufunga hiyo akaunti, utaratibu mwingine wa kupata laini nyingine utafuata.

Muamala wa kimakosa utatokea lakini ni muhimu kutoa ripoti mara moja kwa kupiga huduma kwa wateja kwa namba 100. Kama pesa bado haijatolewa bado, Tigo watweza kubadilisha huo muamala na kurudi kwa mteja. Kama pesa imeshatolewa na mpokeaji, mteja atoe taarifa kituo cha polisi na Tigo wataendelea na utaratibu mwingine wa kurudisha pesa.

Huduma hii ya Zoop inatoa suluhisho la kuondoa urasimu katika malipo ya ada kwa baadhi ya shulle ikiambatana na kukusanya na kutunza kumbukumbu. Malipo yanafanywa  kwa kutumia TigoPesa.

Zoop Tanzania company limited ni moja ya makampuni yaliyoingia makubaliano na taasisi za elimu Tanzania kurahisisha payment ya ada kutumia TIGOPESA. Zoop imesaidia shule nyingi ikiwamo Eagle Boys Secondary School, Heritage English Medium,.Mango School na kadhalika.

Huduma hii inawasaidia wateja wenye mita za zamani za Tanesco kuliopa bili kutumia Tigo Pesa.

  • Piga *150*01#
  • Chagua namba 4 “malipo”
  • Chagua namba 3 "kupata kumbukumbu namba "
  • Chagua namba 3 "chagua kampuni"
  • Kwenye orodha utapata chaguo la kulipa BILI 

Utambulisho wa malipo hutolewa na shule husika ,inaweza kuwa ni namba ya usajili wa mwanafunzi au namba ya utambulisho kutokana na makubaliano ya Zoop na shule.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo